Posts

Showing posts from 2019

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO KIDATO CHA KWANZA 2020

Shule ya sekondari Humura iliyoko wilaya ya muleba mkoa wa kagera umbali wa kilometa 30 kutokea Muleba mjini inawatangazia nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2020.  Shule inayo mandhari nzuri ya kujisomea pia ina walimu waliobobea katika ufundishaji. Inatoa mwanya kwa wasomaji kuwa huru na kufaidi kile wanachokitafuta. Mbali na kuwa na ghalama nafuu pia hutoa masomo ya ziada bila malipo yoyote kwa wanafunzi wote.  Fomu ya kujiunga inapatikana katika link hapa chini Joining instruction form 1 2019 Pia shule inazo nafasi za kuhamia kwa kidato cha II,III na V. Pia inatoa mafunzo kwa wanafunzi wanatafuta credit (re-seaters)  Sisi kwetu Humura elimu ni mwanga Mlete mwanao Humura ushuhudie maajabu yaliyo katika vitendo. Kwa mawasiliano 0754749472 mkuu wa shule   0755 717 597 makamu mkuu wa shule 0753 015 231 Mtaaluma mkuu

PRE-FORM ONE 2019

Image
TANGAZO SHULE YA SEKONDARI HUMURA ILIYOKO RUBYA WILAYANI MULEBA MKOA WA KAGERA INAWATANGAZIA NAFASI ZA MASOMO YA “PRE – FORM ONE” KWA WANAFUNZI WOTE WALIOMALIZA DARASA LA SABA. HII NI KWA AJILI YA KUWAANDAA WANAFUNZI KUJIUNGA NA MASOMO YA SEKONDARI. MASOMO YA PRE – FORM ONE YATAANZA TAREHE 23/9/2019 MPAKA  13/12/2019. GHARAMA YA MASOMO NI SH.40,000/= KWA WANAFUNZI WA KUTWA NA KWA WANAFUNZI WA BWENI WATALIPA SH.140,000/= TU. PIA SHULE INAWATANGAZIA NAFASI ZA MASOMO YA KIDATO CHA KWANZA 2020. NJOO UCHUKUE FOMU YA MAELEKEZO YA KUFANYA MTIHANI WA KUJIUNGA NA SHULE HAPA SHULENI AU TEMBELEA TOVUTI YA SHULE www.humurass.com AU BLOG YA SHULE humurass.blogspot.com  AMBAPO UTAPATA MAELEKEZO ZAIDI. MTIHANI WA KUJIUNGA UTAFANYIKA TAREHE 19/10/2019. KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU NA. 0754749472/0788052090. IMETOLEWA NA UONGOZI WA SHULE YA SEKONDARI HUMURA

HUMURA KIWANDA CHA KUINUA VIPAJI

Image
HUMUARA PACHA WA MICHEZO Baadhi ya wanamichezo wa copa cocacola Shule ya sekondari ya Humura imekuwa mdau mkubwa wa michezo na pia kimekuwa kiwanda cha kuinua vipaji mbali mbali vya kuimba, kucheza na kuigiza.  Njoo na mwanao humura sekondari na hupate kile kilicho zaidi ya unachotegemea KWA MAWASILIANO ZAIDI 0754749472 0762656854

MATOKEO KIDATO CHA SITA 2019

Image
Samare ya matokeo kidato cha sita 2019 Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019 yaliyotangazwa siku ya tarehe 11/7/2019 yamepokelewa kwa furaha sana na uongozi mzima wa shule ya sekondari humura na jumuiya nzima, wanajamii na wanafunzi. Kwani yamekuwa matokeo yakutia faraja na mkombozi kwa vijana hawa ambao kuja humura imekuwa faraja kwani walidhani ndoto zao zilishafutika. Matokeo kwa ujumla shule haina daraja zero (division 0 ) Matokeo kwa ujumla shule ilikuwa na watahiniwa 151  wasichana wakiwa 31 na wavulana 130. Watahiniwa hao wakiwa katika mgawanyo wa michepuo ya HKL,HGK,HGL na CBG. matokeo kuna daraja la kwanza (division I) 38, division II 75, division III 34 na division IV 4. Akiongea baada ya matokeo hayo kutoka mkuu wa shule hiyo ndugu ALMACHIUS MAFIGI ametoa neno la shukrani kwa walimu wote, uongozi wa shule na wazazi pia amewapongeza wanafunzi wote kwa juhudi zao na kuweza kupata matokeo hayo, "Sio kila ndoto inayofifia basi hupotea kabisa ukiwa na nia ya dhati un...

USAJILI KIDATO CHA TANO MWAKA WA MASOMO 2019/2020

Image
Kutoka ofisi ya taaluma humura      Shule ya sekondari Humura inapenda kuwajulisha wazazi na wanafunzi wote kuwa imeanza usajili kwa kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2019/2020. Wanafunzi wote wenye vigezo vya kufanya mtihani wa kidato cha sita yaani akiwa na daraja C kwa masomo matatu. Na asiwe na daraja F kwenye mchepuo wake. Michepuo ambayo inasajiliwa mpaka sasa na ambayo inafundishwa shuleni ni HGK, HKL, HGL na CBG. Pia shule inakaribisha wanafunzi wa kuristi (re-seaters) kidato cha sita nafasi zipo na uhakika wa kupata kile ulichokikosa ni asilimia mia moja. Karibu Humura kisima cha elimu kwetu sifuri na division IV ni mwiko.     Kwa mawasiliano piga simu namba   0754749472    0762656854

PICHA MBALIMBALI ZA SHULE

Image
Shule ya sekondari humura imebarikiwa kuwa na mandhari nzuri kwa wanafunzi na walimu na ina majengo mazuri na yenye kukidhi mahitaji ya kila muhitaji. Hizi ni baadhi ya picha zikionesha baadhi ya madarasa. uoto wa kutosha upo kwa wasomao maabara za jutosha kwa masomo yote ta sayansi baadhi ya ofisi za idara mbalimbali baadhi ya madarasa madarasa utajiri wa maji upo wa kutosha kama ilivyo desturi ya kagera                

Form ya kidato cha Tano 2019

Image
Shule ya secondari humura inakaribisha maombi ya kujiunga kidato cha tano kwa wanafunzi watakaokuwa na vigezo kulingana na mwongozo wa baraza la mitihani Tanzania Fomu ya kujiunga inapatikana katika link hapo chini    

ELIMU BORA NI NINI?

Image
ELIMU BORA NI NINI?   Na Mwalimu wa Sanaa Mitazamo ya wananchi kuhusu elimu bure imebadilika kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka 12 iliyopita: mwaka 2005, zaidi ya nusu ya wananchi (56%) walisema kuwa ‘ni bora elimu itolewe bure kwa watoto wetu, hata kama kiwango cha elimu ni cha chini’. Mwaka 2017, wananchi 9 kati ya 10 (87%) wanasema ‘ni bora tukaongeza viwango vya elimu, hata kama itatulazimu kulipa ada.’ Wananchi 9 kati ya 10 (87%) wangependa serikali itumie fedha kwenye mpango wa kutoa mafunzo na kuwasaidia walimu kuliko kugawa sare za shule bure ikilenga kuwaondolea wazazi mzigo wa kununua sare hizo. Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao   Elimu Bora au Bora Elimu? Elimu waitakayo watanzania . Matokeo ya muhtasari huu yanatokana na takwimu za utafiti wa  Sauti za Wananchi , utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wah...