MATOKEO KIDATO CHA SITA 2019
Samare ya matokeo kidato cha sita 2019 Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019 yaliyotangazwa siku ya tarehe 11/7/2019 yamepokelewa kwa furaha sana na uongozi mzima wa shule ya sekondari humura na jumuiya nzima, wanajamii na wanafunzi. Kwani yamekuwa matokeo yakutia faraja na mkombozi kwa vijana hawa ambao kuja humura imekuwa faraja kwani walidhani ndoto zao zilishafutika. Matokeo kwa ujumla shule haina daraja zero (division 0 ) Matokeo kwa ujumla shule ilikuwa na watahiniwa 151 wasichana wakiwa 31 na wavulana 130. Watahiniwa hao wakiwa katika mgawanyo wa michepuo ya HKL,HGK,HGL na CBG. matokeo kuna daraja la kwanza (division I) 38, division II 75, division III 34 na division IV 4. Akiongea baada ya matokeo hayo kutoka mkuu wa shule hiyo ndugu ALMACHIUS MAFIGI ametoa neno la shukrani kwa walimu wote, uongozi wa shule na wazazi pia amewapongeza wanafunzi wote kwa juhudi zao na kuweza kupata matokeo hayo, "Sio kila ndoto inayofifia basi hupotea kabisa ukiwa na nia ya dhati un...