MATOKEO KIDATO CHA SITA 2019

Samare ya matokeo kidato cha sita 2019

Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019 yaliyotangazwa siku ya tarehe 11/7/2019 yamepokelewa kwa furaha sana na uongozi mzima wa shule ya sekondari humura na jumuiya nzima, wanajamii na wanafunzi. Kwani yamekuwa matokeo yakutia faraja na mkombozi kwa vijana hawa ambao kuja humura imekuwa faraja kwani walidhani ndoto zao zilishafutika. Matokeo kwa ujumla shule haina daraja zero (division 0 )
Matokeo kwa ujumla shule ilikuwa na watahiniwa 151  wasichana wakiwa 31 na wavulana 130. Watahiniwa hao wakiwa katika mgawanyo wa michepuo ya HKL,HGK,HGL na CBG. matokeo kuna daraja la kwanza (division I) 38, division II 75, division III 34 na division IV 4.
Akiongea baada ya matokeo hayo kutoka mkuu wa shule hiyo ndugu ALMACHIUS MAFIGI ametoa neno la shukrani kwa walimu wote, uongozi wa shule na wazazi pia amewapongeza wanafunzi wote kwa juhudi zao na kuweza kupata matokeo hayo, "Sio kila ndoto inayofifia basi hupotea kabisa ukiwa na nia ya dhati unayo nafasi kubwa ya kufufua ndoto yako, napongeza uongozi mzima kwa juhudi zao, wazazi pia nawapongeza wazazi kwa ushirikiano wao" alisema mkuu wa shule.
Shule ya Humura imekuwa na desturi ya kudahili vijana wote walikosa nafasi ya kuchaguliwa katika shule za serikali na kuweza kuwaendeleza na kuwapatia matokeo mazuri, kwani tokea kuanzishwa kwa masomo ya kidato cha tano na sita mwaka 2008 na wahitimu wa kwanza mwaka 2011 hakuna mwanafunzi alishapata daraja sifuri. Hivyo kwetu ushindi ni jadi yetu.
Pia mkuu wa shule alitumia fursa hiyo kuwaimiza wazazi wote wenye watoto wao kuwaleta katika shule ya sekondari humura kwa mwaka wa masomo 2019/2020. Pia kwa watahiniwa wa kujitegemea (Private candidates) wanapokelewa kwa vidato vyote, kidato cha pili (QT) kidato cha nne na sita (PC).
Sisi kwetu elimu ni mwanga na umoja ni nguvu.
Karibuni nyote humura sekondari.
Mawasiliano

  • 0762 656854 TAALUMA
  • 0754 749472 MKUU WA SHULE         

Comments

Popular posts from this blog

PICHA MBALIMBALI ZA SHULE

NAFASI ZA MASOMO KIDATO CHA TANO 2021/2022