NAFASI ZA MASOMO KIDATO CHA TANO 2021/2022

Mkuu wa shule

Shule ya sekondari humura ni shule ya bweni iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera inapenda kuwatangazia nafasi za masomo kwa wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2021/2022. Shule inatoa masomo katika tahasusi (combination) zifuatazo: PCB, CBG, HGL, HGK, na HKL 

 Sifa za mwombaji 

  1. Awe na ufaulu wa kuanzia alama ya C na kupanda juu katika masomo matatu katika mtihani wa kidato cha nne.
  2. Asiwe na alama ya "F" katika tahasusi(combination) anayotarajia kuisoma.
  3. Na iwapo muombaji hana sifa ya 2. Kama ilivyotajwa hapo juu basi atasajiliwa kama private candidate ila ataishi shule na kufundishwa kama wanafunzi wengine wanaofanya kama watahiniwa wa shule

Pia shule ina nafasi za masomo kwa wanafunzi wanaopenda kuhamia kwa kidato cha KWANZA, PILI, TATU NA TANO 

Pia shule ina nafasi za masomo na kituo cha kufanyia mtihani kwa wanafunzi waliokosa credit pass kwenye mitihani yao ya kidato cha nne na sita kwa mwaka wowote wa nyuma, shule inawasajili na kuwawezesha kupata alama hizo kama PRIVATE CANDIDATE na kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Shule ya sekondari humura imekuwa mkombozi wa wanafunzi na fahari ya mzazi kwani inatoa elimu bora kwa gharama nafuu kabisa na kwa kumsikiliza mzazi. 

Ewe mzazi mlete mwanao Humura sekondari kama nawe unahitaji kuwa katika timu ya ushindi kielimu.

Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni.

Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kujiunga piga simu namba hizi 

0754 749 472 mkuu wa shule.

0762 656 854- Taaluma

KARIBU HUMURA SEKONDARI 

ELIMU NI MWANGA


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

PICHA MBALIMBALI ZA SHULE