ELIMU BORA NI NINI?
ELIMU BORA NI NINI? Na Mwalimu wa Sanaa Mitazamo ya wananchi kuhusu elimu bure imebadilika kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka 12 iliyopita: mwaka 2005, zaidi ya nusu ya wananchi (56%) walisema kuwa ‘ni bora elimu itolewe bure kwa watoto wetu, hata kama kiwango cha elimu ni cha chini’. Mwaka 2017, wananchi 9 kati ya 10 (87%) wanasema ‘ni bora tukaongeza viwango vya elimu, hata kama itatulazimu kulipa ada.’ Wananchi 9 kati ya 10 (87%) wangependa serikali itumie fedha kwenye mpango wa kutoa mafunzo na kuwasaidia walimu kuliko kugawa sare za shule bure ikilenga kuwaondolea wazazi mzigo wa kununua sare hizo. Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao Elimu Bora au Bora Elimu? Elimu waitakayo watanzania . Matokeo ya muhtasari huu yanatokana na takwimu za utafiti wa Sauti za Wananchi , utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wah...