Posts

Showing posts from July, 2019

MATOKEO KIDATO CHA SITA 2019

Image
Samare ya matokeo kidato cha sita 2019 Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019 yaliyotangazwa siku ya tarehe 11/7/2019 yamepokelewa kwa furaha sana na uongozi mzima wa shule ya sekondari humura na jumuiya nzima, wanajamii na wanafunzi. Kwani yamekuwa matokeo yakutia faraja na mkombozi kwa vijana hawa ambao kuja humura imekuwa faraja kwani walidhani ndoto zao zilishafutika. Matokeo kwa ujumla shule haina daraja zero (division 0 ) Matokeo kwa ujumla shule ilikuwa na watahiniwa 151  wasichana wakiwa 31 na wavulana 130. Watahiniwa hao wakiwa katika mgawanyo wa michepuo ya HKL,HGK,HGL na CBG. matokeo kuna daraja la kwanza (division I) 38, division II 75, division III 34 na division IV 4. Akiongea baada ya matokeo hayo kutoka mkuu wa shule hiyo ndugu ALMACHIUS MAFIGI ametoa neno la shukrani kwa walimu wote, uongozi wa shule na wazazi pia amewapongeza wanafunzi wote kwa juhudi zao na kuweza kupata matokeo hayo, "Sio kila ndoto inayofifia basi hupotea kabisa ukiwa na nia ya dhati un...

USAJILI KIDATO CHA TANO MWAKA WA MASOMO 2019/2020

Image
Kutoka ofisi ya taaluma humura      Shule ya sekondari Humura inapenda kuwajulisha wazazi na wanafunzi wote kuwa imeanza usajili kwa kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2019/2020. Wanafunzi wote wenye vigezo vya kufanya mtihani wa kidato cha sita yaani akiwa na daraja C kwa masomo matatu. Na asiwe na daraja F kwenye mchepuo wake. Michepuo ambayo inasajiliwa mpaka sasa na ambayo inafundishwa shuleni ni HGK, HKL, HGL na CBG. Pia shule inakaribisha wanafunzi wa kuristi (re-seaters) kidato cha sita nafasi zipo na uhakika wa kupata kile ulichokikosa ni asilimia mia moja. Karibu Humura kisima cha elimu kwetu sifuri na division IV ni mwiko.     Kwa mawasiliano piga simu namba   0754749472    0762656854

PICHA MBALIMBALI ZA SHULE

Image
Shule ya sekondari humura imebarikiwa kuwa na mandhari nzuri kwa wanafunzi na walimu na ina majengo mazuri na yenye kukidhi mahitaji ya kila muhitaji. Hizi ni baadhi ya picha zikionesha baadhi ya madarasa. uoto wa kutosha upo kwa wasomao maabara za jutosha kwa masomo yote ta sayansi baadhi ya ofisi za idara mbalimbali baadhi ya madarasa madarasa utajiri wa maji upo wa kutosha kama ilivyo desturi ya kagera                

Form ya kidato cha Tano 2019

Image
Shule ya secondari humura inakaribisha maombi ya kujiunga kidato cha tano kwa wanafunzi watakaokuwa na vigezo kulingana na mwongozo wa baraza la mitihani Tanzania Fomu ya kujiunga inapatikana katika link hapo chini    

ELIMU BORA NI NINI?

Image
ELIMU BORA NI NINI?   Na Mwalimu wa Sanaa Mitazamo ya wananchi kuhusu elimu bure imebadilika kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka 12 iliyopita: mwaka 2005, zaidi ya nusu ya wananchi (56%) walisema kuwa ‘ni bora elimu itolewe bure kwa watoto wetu, hata kama kiwango cha elimu ni cha chini’. Mwaka 2017, wananchi 9 kati ya 10 (87%) wanasema ‘ni bora tukaongeza viwango vya elimu, hata kama itatulazimu kulipa ada.’ Wananchi 9 kati ya 10 (87%) wangependa serikali itumie fedha kwenye mpango wa kutoa mafunzo na kuwasaidia walimu kuliko kugawa sare za shule bure ikilenga kuwaondolea wazazi mzigo wa kununua sare hizo. Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao   Elimu Bora au Bora Elimu? Elimu waitakayo watanzania . Matokeo ya muhtasari huu yanatokana na takwimu za utafiti wa  Sauti za Wananchi , utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wah...